Ofisi ya Rais - TAMISEMI inapenda kuutangazia Umma kuwa, Serikali
imetoa kibali cha nafasi za ajira ya walimu ili kujaza nafasi wazi
zilizopatikana kutokana na walimu waliofariki, walioacha kazi,
waliofukuzwa utumishi na wastaafu kuanzia kipindi cha Julai, 2018
hadi Juni, 2019. Kwa sababu hiyo, OR-TAMISEMI imeandaa mfumo
wa Online Teacher Employment Application System – OTEAS ambapo
walimu wenye sifa watatuma maombi yao kwa njia ya mtandao
kupitia kiunganishi cha http://ajira.tamisemi.go.tz
Walimu wanaotakiwa kutuma maombi ni wenye sifa za kitaaluma
kama ifuatavyo:
A. WALIMU WATAKAOAJIRIWA SHULE ZA MSINGI
i. Mwalimu Daraja la IIIA – mwenye Astashahada (Cheti) ya ualimu
ii. Mwalimu Daraja la IIIB - mwenye Stashahada (Diploma ya
Ualimu katika masomo ya English, Civics, Historia, Jiografia na
Kiswahili;
iii. Mwalimu Daraja la IIIC - mwenye Shahada ya Ualimu kwa
masomo ya English, Civics, General Studies, History, Geography &
Kiswahili.
iv. Mwalimu Daraja la IIIC - mwenye Mahitaji Maalum aliyehitimu
Shahada ya Ualimu kwa masomo ya English, Civics, General
Studies, History, Geography & Kiswahili.
B. WALIMU WATAKAOAJIRIWA SHULE ZA SEKONDARI
i. Mwalimu Daraja la IIIC – mwenye Shahada ya Ualimu
waliosomea Elimu Maalum;
ii. Mwalimu Daraja la IIIB – mwenye Stashahada (Diploma) ya
Ualimu waliosomea Elimu Maalum;
iii. Mwalimu Daraja la IIIB – mwenye Stashahada ya Ualimu somo la
Physics, Mathematics , Biology & Chemistry;
iv. Mwalimu Daraja la IIIC - mwenye Shahada ya Ualimu somo la
Agriculture Science;
v. Mwalimu Daraja la IIIC – mwenye Shahada ya Ualimu somo la
Home Economics;
vi. Mwalimu Daraja la IIIC - mwenye Shahada ya Ualimu somo la
Physics, Mathematics, Chemistry & Biology;
vii. Mwalimu Daraja la IIIC - mwenye Shahada ya Ualimu somo la
Book Keeping, Commerce, Accounts & Economics; na
viii. Mwalimu Daraja la IIIC – mwenye Shahada ya Ualimu somo la
English, Civics & General Studies.
C. SIFA ZA JUMLA
Waombaji wa nafasi tajwa hapo juu wawe na sifa za jumla zifuatazo:-
i. Awe ni Mtanzania;
ii. Awe amehitimu chuo kinachotambulika na Serikali kati ya
mwaka 2014 hadi 2017; isipokuwa kwa wahitimu wa Elimu ya
Ualimu wa masomo ya Fizikia na Hisabati;
iii. Asiwe na umri wa zaidi ya miaka arobaini na tano (45) wakati wa
kutuma maombi haya;
iv. Walimu waliowahi kutuma maombi na hawajaajiriwa
wanapaswa kutuma maombi upya.
D. MWISHO
Maombi yote yawasilishwe kwa mtandao na yawe na nakala za vyeti
vya taaluma, utaalamu na kuzaliwa. Waombaji wanatakiwa kutuma
maombi yao kuanzia tarehe 27/02/2019 hadi 15/03/2019.
Imetolewa na
Katibu Mkuu
Ofisi ya Rais - TAMISEMI
0 Comments